Unaambiwa Linapokuja suala la kuhakikisha mama wa mwanae Wanaishi kwa furaha, North anapendeza kadri iwezekanavyo, Yeezy hana mkono wa birika. Na ndio maana ametema $250,000 (zaidi ya shilingi milioni 400) kwaajili ya kundi la watu wanaompamba Kim Kardashian ( glam squad).
“Kim anaamini timu yake pekee kumfanya apendeze na hataki kufanya kazi na watu wa nje. Hii si rahisi na Kanye ametoa $250,000 wakati yupo kwenye ziara kwaajili hiyo. Pesa haina maana yoyote kwa Kanye sababu anataka mrembo wake aonekane bomba,” kilisema chanzo hicho.
Inadaiwa kuwa Kanye hachukizwi na matumizi makubwa ya Kim sababu yeye mwenyewe hutumia fedha nyingi mno kwaajili yake.













0 maoni